Translate

Ijumaa, 18 Agosti 2017

Burudika sasa kwa kusikiliza simulizinzur kabisa ya mapenzi kutoka kwa @hadithizetu ndani ya #pillowtalk

Jumatatu, 14 Agosti 2017

Jijengee mazingira ya kusoma, jifunze mengi ya dunia. Pakua KITABU app kwenye playstore yako pata vitabu mbalimbali.
Mtembezi na hadithizetu, wanakuletea simulizi nzuri kabisa ya sirudi nyumbani chini ya utunzi wa Frank david, click here www.mtembezi.co.tz
PENZI LA MKE WA BABA
SEHEMU YA 11
MTUNZI FRANK DAVID
WHATSAPP 0769510060
Kabla baba hajaweka kile chakula kinywani, alisema "mke wangu kila ninapo muona mtoto ulie nizalia najisikia furaha sana moyoni mwangu, nakupenda sana mke wangu" baba aliendelea na kusema kwamba, "mda mwingine nashindwa nikupe zawadi gani ili uone furaha niliyo nayo moyoni" ndipo baba akasema, "achama nikulishe kidogo mke wangu maana upendo umezidi sana kwako" kwakua mama alikuwa ameweka sumu kwenye chakula cha baba ili afe kusudi apate nafasi ya kufanya mapenzi na mimi, mama alikataa kula, baba akasema, "haa! Mke wangu nakulisha hutaki, tatizo nini?" Mama akasema, "hapana mme wangu, chakula changu kinanitosha, wewe kula chako" nikamkonyeza mama ale, kusudi baba asije kunihisi vibaya, lakini mama akakataa kula, maana angekiweka tu mdomoni basi angekufa yeye. Baba alinuna sana kisha akaenda chumbani kwake bila kula, sasa siku hiyo kulikuwa na mvua sana hivyo hali ya hewa ilikuwa ya baridi, ikapelekea mimi kupata hamu ya kula zaidi ndipo nikataka kuchukua chakula cha baba ili nikile mimi kusudi kisimwage, kumbe kwenye chakula kulikuwa na sumu ambayo mama alikuwa ameweka ili baba yangu augue kwa mda mrefu alafu afe, mama akasema "meshack naomba usile hicho chakula" nikamwambia, "niache bhana mimi nina njaa" mama akavuta ile sahani mpaka ikaanguka chini na kupasuka, nilichukia pia ndipo nikatoka sebreni na kwenda kulala chumbani kwangu. Kulipo kucha asubuhi mama yangu akaandaa chai ili aweke ile dawa kusudi baba akinywa tu aanze kuugua mpaka kufa, sasa mama alipo weka chai kwenye kikombe cha kwanza, bahati mbaya kilianguka chini na kupasuka, mama akaweka kikombe cha pili akajitingisha mwenyewe kikapasuka pia, wakati anaweka kikombe cha tatu baba akasema, "mke wangu acha tu sitaki chai yako maana nitakumalizia vikombe, nitakunywa chai kazini" mama alichukia, maana mipango yake yote ilikuwa inakwama, ndipo akarudi kwa bibi alie kuwa anampa dawa, mama akaambiwa kuwa achukue tunda la peazi kisha akapewa maelekezo ya kupaka dawa ili baba akila afe, kweli baba alipo kula lile peazi alianza kuteseka, alikuwa mnyonge, baba alikuwa hali chakula, mda wote anatapika tu, rangi ya mwili wa baba ikabadilika, kumbe lile peazi lilikuwa linaota tumboni mwa baba kichawi.

KIFO CHA KISU

Soma hadithi hii ya kusisimua iliyojaa mafundisho mazuriya kimaisha katika jamii inayotuzunguka...usipitwe na mkasa huu


KITABU APP


Soma vitabu vyetu vya hadithi tamu na za kusisismua za FRANK DAVID kupitia app yetu ya kitabu

Burudika sasa kwa kusikiliza simulizinzur kabisa ya mapenzi kutoka kwa @hadithizetu ndani ya #pillowtalk