PENZI LA MKE WA BABA
SEHEMU YA 11
MTUNZI FRANK DAVID
WHATSAPP 0769510060
Kabla baba hajaweka kile chakula kinywani, alisema "mke wangu kila
ninapo muona mtoto ulie nizalia najisikia furaha sana moyoni mwangu,
nakupenda sana mke wangu" baba aliendelea na kusema kwamba, "mda
mwingine nashindwa nikupe zawadi gani ili uone furaha niliyo nayo
moyoni" ndipo baba akasema, "achama nikulishe kidogo mke wangu
maana upendo umezidi sana kwako" kwakua mama alikuwa ameweka sumu
kwenye chakula cha baba ili afe kusudi apate nafasi ya kufanya mapenzi
na mimi, mama alikataa kula, baba akasema, "haa! Mke wangu nakulisha
hutaki, tatizo nini?" Mama akasema, "hapana mme wangu, chakula changu
kinanitosha, wewe kula chako" nikamkonyeza mama ale, kusudi baba asije
kunihisi vibaya, lakini mama akakataa kula, maana angekiweka tu mdomoni
basi angekufa yeye. Baba alinuna sana kisha akaenda chumbani kwake bila
kula, sasa siku hiyo kulikuwa na mvua sana hivyo hali ya hewa ilikuwa ya
baridi, ikapelekea mimi kupata hamu ya kula zaidi ndipo nikataka
kuchukua chakula cha baba ili nikile mimi kusudi kisimwage, kumbe kwenye
chakula kulikuwa na sumu ambayo mama alikuwa ameweka ili baba yangu
augue kwa mda mrefu alafu afe, mama akasema "meshack naomba usile hicho
chakula" nikamwambia, "niache bhana mimi nina njaa" mama akavuta ile
sahani mpaka ikaanguka chini na kupasuka, nilichukia pia ndipo nikatoka
sebreni na kwenda kulala chumbani kwangu. Kulipo kucha asubuhi mama
yangu akaandaa chai ili aweke ile dawa kusudi baba akinywa tu aanze
kuugua mpaka kufa, sasa mama alipo weka chai kwenye kikombe cha kwanza,
bahati mbaya kilianguka chini na kupasuka, mama akaweka kikombe cha pili
akajitingisha mwenyewe kikapasuka pia, wakati anaweka kikombe cha tatu
baba akasema, "mke wangu acha tu sitaki chai yako maana nitakumalizia
vikombe, nitakunywa chai kazini" mama alichukia, maana mipango yake yote
ilikuwa inakwama, ndipo akarudi kwa bibi alie kuwa anampa dawa, mama
akaambiwa kuwa achukue tunda la peazi kisha akapewa maelekezo ya kupaka
dawa ili baba akila afe, kweli baba alipo kula lile peazi alianza
kuteseka, alikuwa mnyonge, baba alikuwa hali chakula, mda wote anatapika
tu, rangi ya mwili wa baba ikabadilika, kumbe lile peazi lilikuwa
linaota tumboni mwa baba kichawi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni